Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Kizalendo, BNP nchini Bangladesh, Tarique Rahman amerejea nyumbani baada ya karibu miaka 17 na hivyo kuwapa nguvu wafuasi wa chama hicho. Rahman anatarajiwa kuwa mgombea mwenye nafasi ya juu ya kuwa waziri mkuu katika uchaguzi utakaofanyika mnamo mwezi Februari.

Maelfu kwa maelfu ya wafuasi walijipanga kutoka uwanja wa ndege wa Dhaka hadi ukumbi wa mapokezi, wakipeperusha bendera za chama na wakiwa wamebeba mabango na maua, huku wakiimba kaulimbiu za kumkaribisha Rahman.Viongozi wakuu wa chama chake wamempokea kwenye uwanja wa ndege chini ya ulinzi mkali. Uchaguzi huo wa mwezi Februari unazingatiwa kuwa muhimu katika kurejesha utulivu wa kisiasa nchini Bangladesh.

Mandhari ya kisiasa yamebadilika nchini humo tangu kuondolewa madarakani kwa waziri mkuu Sheikh Hasina. Tarique Rahman ni mwana wa Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Khalida Zia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *