Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana leo katika sikukuu ya Krismasi, hali inayoashiria kuendelea kwa mapigano licha ya siku hiyo kuwa ya amani kwa waumini wa dini ya Kikristo.

Ripoti kutoka Ukraine zinaeleza kuwa mashambulio hayo yameendelea kulenga maeneo ya raia, na kuzua hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.

Kwa mujibu wa polisi wa Ukraine, shambulio la ndege zisizo na rubani lililotokea katika mji wa Chernihiv limepiga jengo la makazi la ghorofa tano, ambapo mtu mmoja amefariki dunia na watu wengine watano wamejeruhiwa.

Polisi wamesema wnaendelea na shughuli za uokoaji na uchunguzi katika eneo la tukio ili kubaini kiwango cha uharibifu na kuwahudumia waathirika.

#azamtvupdates
Mhariri: @rajjmsangi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *