ARUSHA: NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa amesema wananchi wote  waliojenga maeneo ambayo barabara ya Siha wilayani Hai mkoani Kilimanjaro hadi Longido mkoani Arusha itakapopita watalipwa fidia kupisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami.

Dk Kiruswa alisema hayo akiw kata ya Tingatinga wilayani Longido na kuongeza kuwa serikali iko katika hatua ya tathmini ya wale walipitiwa na mradi huo ili waweze kulipwa fidia kwa barabara hiyo yenye urefu wa km 56 ni faida kibiashara kwa wakazi wa Longido na Siha.

Aliwatoa wasiwasi kuwa hakuna atakayenyimwa fidia kupisha mradi huo na kusema kuwa kinachopaswa kwa wakazi wa Tingatinga kushirikiana na serikali ili watakaolipwa fidia ni wale tu watakaopitiwa na mradi huo.

Akizungumzia mradi wa maji aliochangia Sh milioni 9.5 kwa ununuzi wa mabomba ya maji kwa ajili ya kuunganisha toka bomba kuu la mradi maji wa Mto Simba hadi Longido,Dk Kiruswa aliwataka wakazi hao kuharakisha uchimbaji wa mtaro wa kupitisha mabomba ya maji hadi vijijini kwa ajili ya watu na mifugo na aliwataka mradi huo kukamilika mwaka huu.

Dk Kiruswa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Longido aliwahimiza wananchi kumpa ushirikiano Diwani Peter Lekanet ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido kumpa ushirikiano ili kuleta maendeleo katika kata hiyo kwani diwani huyo ni muadilifu,msikivu na mfuatiliaji hivyo wamepata jembe kwa maendeleo ya kata hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido,Thomas Ngobei amesema miaka mitano ya uongozi wao ni mwaka wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyobuniwa na serikali kuu na halmashauri na atakayekwamisha katika utekelezaji huyo sio mwenzao itabidi awapishe kwani hana nia njema na Jimbo la Longido.

Ngobei alisema Baraza la Madiwani limejipanga kila diwani kuorodhesha changamoto zake katika kata na zitakuwa zikitatuliwa kwa kila mwaka na ndani ya miaka mitano ana uhakika Longido itakuwa imepaa kimaendeleo na wananchi wataifurahia serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Naye, Diwani Lekanet amewataka wananchi wa kata ya Tingatinga kujitoa kwa wingi katika uchimbaji mtaro wa maji ili shughuli za kuvuta maji toka bomba kuu hadi vijijini ukamilike kwa wakati kama Mbunge alivyokusudia kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo na alisema wale waliovamia kata hiyo toka kukimbia ukame katika vijiji vya Ngerenyani, Engikaret na Monduli walipokelea bila kutozwa chochote tofauti na watu wanavyopotosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *