#HABARI: Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Shinyanga wametumia Sikukuu ya Krismasi kusherehekea pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali mkoani humo.

Katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Mboni Mhita, amewahimiza wazazi na walezi kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji wakiwemo watoto yatima, watu wasiojiweza na wajane.

Bi. Mhita ameyasema hayo wakati akisherehekea sikukuu ya Krismasi na watoto yatima pamoja na walezi wao nyumbani kwake eneo la Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi, amesema Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia bado linapokea kesi nyingi za unyanyasaji wa watoto, hasa watoto wa kike ambapo ameonya wananchi kuacha vitendo vinavyokiuka utu na haki za binadamu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *