#HABARI: Waumini wa Kanisa Katoliki nchini, wametakiwa kusimamia maadili kuanzia ngazi ya familia, kudhibiti matumizi ya simu za mkononi na kuepuka tabia zinazoharibu ustawi wa kifamilia ikiwamo ulevi wa kupindukia, ili kulinda umoja, afya na mustakabali wa jamii.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Maonano Mawela Jimbo la Moshi, ambaye pia ni Vikari wa Vikariati ya Jimbo hilo Padre Patrick Soka, ametoa wito huo wakati akizungumza baada ya ibada ya Noeli.
Padre Soka amesema matumizi ya simu ndani ya familia yanapaswa kudhibitiwa hususan wakati wa kula na nyakati za vikao vya kifamilia, ili kuruhusu mazungumzo ya ana kwa ana yatakayojenga ukaribu, kusaidia kusikilizana na kutatua changamoto zinazowakabili wanajamii.
Aidha, amelaani tabia ya baadhi ya watu kutoka mikoani kuwashindanisha vijana kunywa pombe kali, akibainisha kuwa ulevi huo umeharibu maisha ya vijana wengi, kupunguza nguvu kazi, kuzalisha migogoro ya kifamilia na kusababisha vifo.
Amesisitiza kuwa kama mtu atalazimika kutumia pombe basi afanye hivyo kwa kiasi, huku akiwakumbusha wanaume wanaorejea majumbani usiku wa manane wakiwa wamelewa kuacha tabia hiyo kwa kuwa imekuwa chanzo cha hofu kwa watoto na kuvuruga malezi.
Katika hatua nyingine, Padre Soka amewataka waumini kuacha mila za kuchinja wanyama kwa ajili ya matambiko, akisema hazina maana yoyote na mara nyingi nyama hizo huishia kuwa chakula cha mbwa, badala yake wanyama wachinjwe kwa matumizi halali ya chakula.
Amesisitiza pia umuhimu wa waumini kushiriki ibada, kuishi kwa upendo, kujenga amani kuanzia ngazi ya familia na kuendelea kuiombea nchi, kwa kuwa kupotea kwa amani kunaleta madhara makubwa kwa jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania