
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imethibitisha kuwa Marekani imefanya ‘mashambulizi ya uhakika dhidi ya maeneo lengwa ya kigaidi nchini Nigeria kwa mashambulizi ya anga’ baada ya Rais Donald Trump kutangaza operesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu. Katika katika taarifa yake wizara hiyo ilisema mamlaka za Nigeria zinaendelea kushirikiana kwa mpangilio na washirika wa kimataifa, ikiwemo Marekani, katika kukabiliana na tishio la kudumu la ugaidi na misimamo mikali ya vurugu Taarifa iliongeza kuwa mashambulizi hayo yamefanyika kwa usahihi dhidi ya malengo ya kigaidi nchini Nigeria kwa mashambulizi ya anga, katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.