Maduka na mikahawa katika jiji la Uswizi la Lugano ambayo sasa inakubali Bitcoin

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    • Author, John Lawrenson
    • Nafasi, Economics Correspondent – Lugano, Switzerland
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Katika mgahawa wa chakula unaotazama ziwa na kuzungukwa na milima, katikati ya mji wa Lugano nchini Uswisi, mteja anaagiza kahawa na kuuliza kama anaweza kulipa kwa sarafu ya Bitcoin.

Mhudumu anamkabidhi kifaa kinachofanana na mashine ya kulipia kwa kadi ya benki, lakini kwa hakika ni kifaa cha malipo ya sarafu ya kidijitali.

Baraza la jiji la Lugano liligawa vifaa hivyo bila malipo kwa maduka na migahawa ya eneo hilo. Mnunuzi analipa kwa njia ya kielektroniki kupitia pochi ya Bitcoin kwenye simu yake. Kiasi kinacholipwa ni Bitcoin 0.00008629, sawa na takribani dola 8.80 za Marekani.

Kwa wengi, Bitcoin huonekana zaidi kama uwekezaji au kamari ya kifedha, si kama njia ya kununua bidhaa za kawaida. Hata hivyo, mjini Lugano, eneo linalozungumza Kiitaliano nchini Uswisi hali ni tofauti. Ingawa faranga za Uswisi bado ndizo sarafu kuu, takribani maduka na migahawa 350 sasa yanakubali malipo kwa Bitcoin.

Zaidi ya hayo, mamlaka za jiji zimeanza kuruhusu malipo ya sarafu za kidijitali kwa baadhi ya huduma za umma. Ada za chekechea, kwa mfano, zinaweza kulipwa kwa Bitcoin.

Pia unaweza kusoma:

Katika mgahawa wa McDonald’s, nilizungumza na Nicolas, raia wa Ufaransa ambaye anaamini kwa dhati katika Bitcoin. Anasema ”Faida kubwa ya Bitcoin ni uhuru unaoambatana nayo, kwa kuwa huniwezesha mtumiaji kujiondoa kwenye mifumo ya kifedha inayotegemea madalali na ada nyingi”.

Nicolas anaeleza kuwa nchini Uswisi kuna kadi maalumu za Bitcoin zinazofanya kazi kama kadi za zawadi. Mtu hununua kadi kwa faranga za Uswisi, kisha kiasi hicho huwekwa kwenye pochi ya kidijitali ya Bitcoin kwenye simu.

Nilipotembea katika barabara kuu ya kibiashara katikati ya Lugano, nilikuta maduka mengi yakijishughulisha na bidhaa za kifahari kama vito na mavazi ya bei ghali.

Katika duka la Vintage Nassa, linalouza mifuko na saa mpya na zilizotumika, mmiliki wake, Cherubino Frey, anasema anakubali Bitcoin kwa sababu ada zake za miamala ni ndogo kuliko zile za kadi za benki.

Kwa kawaida, ada za malipo kwa Bitcoin huwa chini ya asilimia moja. Kwa kulinganisha, ada za kadi za deni zinaweza kufikia asilimia 1.7, huku kadi za mkopo zikifikia asilimia 3.4, ingawa viwango hivi hutofautiana kati ya nchi.

Hata hivyo, nilimuuliza Frey iwapo biashara yake inakubali sarafu ya bitcoin, anasema bado lakini anakiri kuwa kwa sasa wateja wachache ndio hutumia Bitcoin. Anaamini matumizi yake yataongezeka polepole, ”kama mti unaokua taratibu hadi kufikia ukubwa mkubwa baada ya miaka kadhaa”.

Karibu na duka lake, nilitembelea makao makuu ya mpango wa Plan B, ulioanzishwa mwaka 2022 na jiji la Lugano kwa ushirikiano na jukwaa la sarafu za kidijitali la Tether. Lengo la mpango huo ni kuelimisha umma kuhusu sarafu za kidijitali na kuifanya Lugano kuwa kitovu cha Bitcoin barani Ulaya.

Watu wanaolipa kwa kutumia Bitcoin kupitia programu kwenye simu zao

Karibu na duka lake, nilitembelea makao makuu ya mpango wa Plan B, ulioanzishwa mwaka 2022 na jiji la Lugano kwa ushirikiano na jukwaa la sarafu za kidijitali la Tether.

Ikiwa nembo ya ‘B’ inasimamia neno Bitcoin, lengo la mpango huo ni kuelimisha umma kuhusu sarafu za kidijitali na ”kuifanya Lugano kuwa kitovu cha Bitcoin barani Ulaya”.

“Nataka kuzungumzia changamoto niliokuwa nazo Julai iliyopita,” anasema mkurugenzi wa mpango wa Plan B, Mire Lebouni.Anasema alipata tatizo la benki lililomzuia kutumia fedha zake. Kwa siku 11, alilazimika kutumia Bitcoin pekee kama njia ya malipo. Anasema uzoefu huo ulimthibitishia kuwa mtu anaweza kuishi Lugano akitegemea Bitcoin, ingawa bado kuna mapungufu.

Mafanikio, changamoto na mitazamo tofauti

Kwa sasa, haiwezekani kulipia usafiri wa umma, mafuta ya magari, au bili za nishati kwa Bitcoin. Hata hivyo, anasema huduma za msingi kama chakula zinapatikana kwa urahisi, na hata hupelekwa hadi nyumbani. Pia kuna vituo vingi vya afya, ingawa madaktari wa meno bado hawajakubali mfumo huo.

Lebouni anatazamia siku zijazo zenye uchumi wa mzunguko, ambapo watu hupata kipato kwa Bitcoin, huihifadhi, huitumia kununua bidhaa, na kulipia huduma mbalimbali.

Si miradi yote ya Bitcoin imefanikiwa kama ya Lugano. Mwaka 2021, El Salvador ilifanya Bitcoin kuwa sarafu halali pamoja na dola ya Marekani. Ili kuhamasisha matumizi yake, serikali iliwapa wananchi kiasi cha Bitcoin chenye thamani ya dola 30. Hata hivyo, wengi walibadilisha Bitcoin hiyo kuwa dola na kuacha kuitumia.

Vincent Charles, rais wa kampuni ya Unchain Data, anasema alipoitembelea El Salvador aligundua kuwa Bitcoin haikutumika sana katika maisha ya kila siku, na wafanyabiashara wachache tu waliikubali.

Hata hivyo, kuna mifano mingine ya mafanikio duniani. Ripoti ya Aprili ilitaja mji mkuu wa Slovenia, Ljubljana, kuwa mji unaoongoza kwa matumizi rafiki ya sarafu za kidijitali, ukifuatiwa na Hong Kong na Zurich.

Cherubino Frey, mmiliki wa duka, anatarajia ukuaji mkubwa wa matumizi ya Bitcoin.

Lucia, mkazi wa eneo hilo ambaye alikuwa akipita, alisema: “Inatamaushwa kwa sababu Pamoja na hayo, si wakazi wote wa Lugano wanaounga mkono Bitcoin. Sanamu ya Satoshi Nakamoto, jina la kubuni la mvumbuzi wa Bitcoin, iliyokuwa kando ya Ziwa Lugano, iliharibiwa mwezi Agosti na kutupwa majini. Tukio hilo liliibua mjadala kuhusu mtazamo wa jamii kwa sarafu za kidijitali.

Lucia, mkazi wa eneo hilo, anasema ana wasiwasi kuhusu sarafu hizi, akizihusisha na uhalifu, mtandao wa giza na upotevu wa fedha kwa wawekezaji wasiokuwa waangalifu.

ATM nchini Uswizi huruhusu watu binafsi kubadilisha faranga za Uswisi hadi Bitcoin.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Profesa wa uchumi Sergio Rossi kutoka Chuo Kikuu cha Fribourg anaonya kuwa Bitcoin ina hatari kubwa kutokana na mabadiliko makali ya thamani yake. Anashauri wafanyabiashara kubadilisha mara moja Bitcoin wanayopokea kuwa sarafu rasmi kama faranga za Uswisi.uharibifu si jambo la kawaida sana hapa. Tabia za watu kwa kawaida ni nzuri sana. Na huoni watu wengi wenye misimamo mikali sana ya kisiasa.”

Lakini alisema alikuwa na mashaka juu ya sarafu-fiche kwa ujumla.

Alibainisha kuwa “watu wengi hupoteza pesa zao kwa sababu wanawekeza katika sarafu za siri na kisha zinaanguka.”

Pia anabainisha hatari ya sifa, kwani sarafu za kidijitali zinaweza kuhusishwa na shughuli haramu, jambo linaloweza kuathiri taswira ya jiji na taasisi zake za kifedha. Aidha, anaonya kuwa ikiwa jukwaa la kidijitali linalohifadhi pochi ya mtumiaji litafilisika, fedha zinaweza kupotea kabisa.

Anaongeza: “Kinyume chake, nchini Uswisi, amana zote za benki zinahakikishiwa hadi faranga 100,000 za Uswisi (dola 125,000). Hii ina maana kwamba ikiwa benki ambayo akiba yangu inahifadhiwa itafilisika, ninaweza kuzirejesha hadi kufikia kiwango hicho.”

Kwa upande wake, meya wa Lugano, Michele Voletti, anasema hana hofu kuwa jiji lake linavutia fedha za uhalifu. Anasema pesa taslimu, kama Bitcoin, zinaweza kutumika kwa mema au mabaya, lakini wahalifu mara nyingi hupendelea pesa taslimu kwa sababu ni rahisi kuficha.

Anaongeza kuwa Bitcoin inasalia kuwa maendeleo chanya kwa jiji la Lugano, na kwamba kampuni 110 za sarafu ya crypto sasa zimehamia jiji hilo au zimeanza kufanya kazi huko.

Soma pia:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *