Mnamo Oktoba 26, jiji la Sudan la El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Kaskazini mwa Darfur, lilianguka mikononi mwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) baada ya miezi kadhaa ya vizuizi na mapigano makali. Miezi miwili baadaye, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yana wasiwasi kuhusu hatima ya raia wanaoishi chini ya udhibiti wa wanajeshi wa Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana pia kama “Hemedti.”

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mauaji ya kikatili, ubakaji, mateso, utekaji nyara… Ingawa makumi ya maelfu ya mashahidi waliokimbia wakati na baada ya kuanguka kwa El-Fasher wametoa maelezo ya kutisha ya siku zilizofuata Oktoba 26, jambo moja lisilojulikana sasa linasababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa waangalizi wa kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita “mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.” Baada ya kuzimwa kwa mitandao, taarifa chache zinatoka katika mji mkuu wa Kaskazini mwa Darfur.

Kulingana na shirika la Madaktari wa Sudan, karibu watu 19,000 kwa sasa wanashikiliwa Nyala, mji ulioko kilomita 200 kusini mwa El-Fasher, makao makuu ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). “Hawa ni wanajeshi, maafisa wa polisi…,” anaelezea Dkt. Mohamed Faisal, mwanachama wa shirika la Madaktari wa Sudan, akihojiwa na Alexandra Brangeon, “lakini angalau 5,000 kati ya wafungwa hawa pia ni raia, waliorudishwa kutoka El-Fasher baada ya shambulio la mwisho la mwezi Oktoba.”

Kuna wanajeshi, maafisa wa polisi… lakini angalau 5,000 kati ya wafungwa hawa ni raia, ambao walirudishwa kutoka El-Fasher wakati wa shambulio la mwisho la mwezi Oktoba. Kuna magereza mawili rasmi huko Nyala: Degrif na Kober. Lakini, kwa kuongezea, RSF hutumia majengo mengi ya raia kama vituo vya kizuizini: nyumba, shule. Baadhi ya raia hawa waliokamatwa ni wanafamilia wa wanajeshi na polisi. Wake na watoto wao wanatuhumiwa kusaidia jeshi la Sudan. Pia wamewakamata familia nyingi za wanajeshi huko Kordofan. Miongoni mwa wengine ni watu mashuhuri, waandishi wa habari, na madaktari. Tuliweza kuhesabu wafanyakazi 73 wa afya. Madaktari wengi walichukuliwa mateka huko El-Fasher, na RSF imedai fidia kutoka kwa familia zao. Wanajeshi wanatumia wafungwa hawa raia kama chanzo cha ufadhili.

Kulingana na daktari huyo, wengi wa wafungwa ni wanafamilia wa vikosi vya usalama na maafisa wa idara za usalama wa Sudan, ambao mara nyingi wanatuhumiwa kuunga mkono jeshi. “Lakini pia kuna waandishi wa habari na madaktari,” anasema Dkt. Mohamed Faisal. “Tumehesabu wafanyakazi 73 wa afya, na madaktari wengi wamechukuliwa mateka huko El-Fasher, huku RSF wakidai fidia kutoka kwa familia zao ili waachiliwe.”

Taarifa kutoka El-Fasher mara nyingi hazijakamilika. Hadi leo, hakuna idadi kamili ya vifo iliyotangazwa. Kulingana na Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale, watu elfu kadhaa wameuawa tangu jiji hilo lilipoanguka mikononi mwa RSF. Picha za setilaiti kutoka angani zilionyesha madoa ya damu ardhini, ushahidi wa mauaji hayo.

Hali mbaya ya kibinadamu

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakitoa wito mara kwa mara wa kufunguliwa kwa njia ya kibinadamu. Mnamo Desemba 20, Waziri Mkuu wa serikali ya Sudan, Kamil Idris, alisafiri hadi New York kukutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa, lakini matokeo ya majadiliano bado hayajulikani.

“Inaonekana kwamba watu wachache sana wamebaki El-Fasher,” anasema Caroline Bouvard, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Solidarity International nchini Sudan, akizungumza na David Baché, “lakini kwa sasa, hakuna shirika lisilo la kiserikali, wala Umoja wa Mataifa wala shirikala Msalaba Mwekundu, ambalo limeweza kufika katika mji huo, kwa hivyo ni vigumu kupata picha iliyo wazi.”

Leo, watu wengi waliolazimishwa kuingia barabarani wamekimbilia katika kambi zinazozunguka mji wa Tawila, kama kilomita 50 magharibi mwa El-Fasher, ambazo huwahifadhi karibu watu 800,000 kati yao wakiwa katika hali duni. “Tunakadiria kwamba tunashughulikia takriban 40% ya mahitaji ya maji,” anaeleza Caroline Bouvard, “na ingawa usambazaji wa chakula ni wa kawaida, tunakabiliwa na viwango vya juu sana vya utapiamlo, haswa miongoni mwa watoto.”

Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi. Kwa msimu wa mvua kuisha, mashirika ya kibinadamu yana wasiwasi kuhusu hatima ya watu 800,000 waliokimbia makazi yao katika miezi ijayo. “Makazi yao, yaliyojengwa kwa majani na maturubai machache ya plastiki, hushika moto mara tu joto linapoanza,” anaonya mkurugenzi wa shirika la Solidarity International nchini Sudan. “Katika wiki za hivi karibuni, moto kadhaa umeathiri zaidi ya familia mia moja kwa jumla.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *