Mwanamume wa Kipalestina amewaua watu wawili, mwanamke na mwanamume, kaskazini mwa Israel leo Ijumaa, Desemba 26, kabla ya kujeruhiwa na risasi, idara ya huduma za dharura ya Israel na polisi wametangaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa akiendesha gari lake, alimgonga mwanamume mwenye umri wa miaka 68 huko Beit She’an kabla ya kumdunga kisu mwanamke mmoja huko Ein Harod, polisi imesema katika taarifa.

Waathiriwa wote wawili wamefariki kutokana na majeraha waliyoyapata, Magen David Adom (MDA), sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel, limetangaza.

Idara ya Huduma za Dharura pia imeripoti kwamba mvulana wa miaka 16 amejeruhiwa kidogo huko Beit Shean baada ya kugongwa na gari. Kufuatia uingiliaji kati wa mpita njia, mshukiwa alipigwa risasi huko Afula na kisha kupelekwa hospitalini, polisi imesema. Jeshi la Israel lilmesema kwamba mshambuliaji alikuwa nchini humo kinyume cha sheria, baada ya kuingia humo siku kadhaa zilizopita. Waziri wa Ulinzi Israel Katz ameagiza jeshi kuchukua hatua kali dhidi ya kijiji cha mshambuliaji.

Mashambulizi kadhaa yamefanywa nchini Israel na Wapalestina tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, ambavyo vilianza na shambulio la kundi la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, katika ardhi ya Israel. Vurugu pia zimeongezeka katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Siku ya Alhamisi, jeshi la Israel liliripoti matukio mawili yanayomhusisha askari wa akiba aliyegonga kwa gari lake Mpalestina aliyekuwa akisali kando ya barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *