
Kupitia mitandao ya kijamii Zelensky ameandika wameafikiana kufanya mkutano wa ngazi ya juu ambapo mambo mengi yanaweza kuamuliwa kabla ya Mwaka Mpya. Kauli hiyo imejiri baada ya duru ya hivi karibuni ya mazungumzo kati ya timu za Marekani na Ukraine kuzaa mpango wa vipengele 20 wa kumaliza vita, ambao tayari umefika kwa mamlaka ya Moscow ili kutathminiwa.Mpango huo unakusudia kuzuia mapigano na kuondoa sharti la Kyiv kuachana rasmi na azma yake ya kujiunga na NATO. Na kiongozi huyo wa Ukraine pia alionyesha kuwa mpango huo unafungua njia ya kuondoa wanajeshi wake katika eneo la mashariki la Donetsk na kuanzisha ukanda usio na silaha, mambo ambayo serikali ya Kyiv hapo awali ilikuwa haiko tayari kuyakubali.