“Kupitia amani, haki za kidemokrasia na uhuru wa kuchagua viongozi, Somalia inaweka msingi wa maendeleo ya muda mrefu — kukuwa kwa uchumi, ustawi wa jamii, na mafanikio kwa taifa,” alisema.

Hongera kwa hatua muhimu

Mabalozi wa Somalia kote duniani wamempongeza Rais Hassan Sheikh Mohamud, serikali na raia kwa hatua hiyo muhimu.

Ubalozi wa Somalia nchini Uturuki umesisitiza kuwa mafanikio ya usalama kwa siku hiyo yamedhihirisha dhamira ya mataifa yote mawili na ushirikiano wa kimataifa.

“Kama taifa mabalo wakati mmoja lilitambulika kwa makabidhiano ya amani ya madaraka, tumechukuwa hatua muhimu kurudisha urithi huo,” balozi huyo alisema.

Ubalozi wa Somalia nchini Tanzania pia ulituma pongezi zake kwa uchaguzi wa amani katika mji mkuu wa nchi.

Katika taarifa, iliitaja siku hiyo kama siku ya ushindi kwa utashi wa taifa. Ubalozi huo pia unawakilisha Somalia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia unahudumia mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Rwanda,Visiwa vya Comoro, na Mauritius.

“Hii ni siku ya kihistoria kwa Somalia, kwa kuwa taifa letu linafanya uchaguzi wake kwa njia ya amani huku raia wakihusika moja kwa moja katika kipindi cha zaidi ya miaka 57,” taarifa hiyo ilisema.

Ubalozi huo ulielezea mafanikio ya uchaguzi huo kutokana na “uthubutu wa watu wa Somalia” na “uongozi imara” wa Rais Mohamud.

“Mafanikio haya yanaonesha hatua ya dhati ya kurudi kwenye demokrasia, uthabiti na maendeleo kwa taifa letu tunalolipenda,” ubalozi ulieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *