Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameweka wazi maelekezo aliyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenda kugusa Jeshi la Polisi ambapo mabadiliko makubwa yakidhamiriwa ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuweza kurejesha mahusiano mazuri na wananchi huku akiweka wazi mabadiliko hayo kuwa ni kulibadili Jeshi la Polisi kutoka matumizi ya nguvu na kuwa Jeshi la Kutoa Huduma na Urekebishaji wa Sheria katika suala la ukamataji wa watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.
Amesema hayo,wakati wa mahojiano maalumu ambapo pia ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini iliyoongozwa na Mwenyekiti Mh. Jaji Mohamed Othman Chande iliyoundwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Januari 2023.