Asasi mbili za Kipalestina yametangaza kwamba, zaidi ya mateka na wafungwa 9,300 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza na vituo vya kuzuiliwa vya Israel wanakabiliwa na “mateso yaliyopangwa.”

Shirika la Masuala ya Mateka na Waachiliwa Huru wa Kipalestina lenye mfungamano na Harakati ya ukombozi wa Palestina pamoja na Klabu ya Wafungwa wa Palestina yametangaza katika taarifa kwamba, Wapalestina hao wanakabiliwa na “ongezeko linaloendelea la hatua za ukandamizaji” katika magereza ya Kizayuni, ikiwa ni pamoja na kupigwa, matumizi ya mabomu ya kushtua, mbwa wa polisi, mshtuko wa umeme, na kunyimwa haki ya wafungwa kupata hewa safi na mahitaji ya msingi, ikiwa ni pamoja na chakula, huduma ya matibabu, na mavazi.

Taarifa hiyo pia inaripoti kuhusu kuimarika kwa ukandamizaji, matumizi ya viboko, gesi, na fimbo, na mwendelezo wa sera ya njaa na kunyimwa matibabu, ambayo imeathiri moja kwa moja afya za wafungwa, haswa wale wanaougua magonjwa sugu, katika magereza ya “Gilboa” na “Shita”.

Asasi mbalimbali za kieneo na kimataifa zimekuwa zikilaani vikali mauaji ya makusudi na mateso ya Wapalestina walioko katika magereza ya kuogofya ya utawala haramu wa Israel, ikiyataja kama “uhalifu kamili wa kivita” na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya uhalifu huo.

Magereza ya kuogofya ya utawala haramu wa Israel yamegeuzwa kuwa viwanja vya mauaji ya moja kwa moja ili kuangamiza Wapalestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *