.

Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock

Rais wa
Ukraine Volodymyr Zelensky amesema atakutana na mwenzake wa Marekani Donald
Trump huko Florida siku ya Jumapili, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu
kukomesha vita vya Urusi.

Zelensky
alisema alitarajia mkutano huo uzingatie mpango wa amani unaosimamiwa na
Marekani, na mapendekezo tofauti ya dhamana za usalama za Marekani. Lakini
afisa mmoja mwandamizi wa Urusi alisema mpango huo ulikuwa “tofauti
kabisa” na ule uliokuwa ukijadiliana na Marekani.

Urusi imezungumzia “maendeleo ya polepole lakini thabiti” katika mazungumzo ila haijatoa
maoni yoyote kuhusu ofa ya Zelensky ya kuondoa wanajeshi kutoka eneo la
mashariki mwa Donbas la Ukraine, ikiwa Urusi pia itajiondoa.

Jumamosi
usiku, milipuko ilisikika huko Kyiv, katika kile maafisa wa Ukraine walisema ni
shambulio jipya la angani la Urusi.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *