.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United inafikiria kumsajili James Garner, Chelsea wanataka kuwaondoa Raheem Sterling, Axel Disasi na Sandro Tonali wanalengwa na Juventus.

Manchester United wanafikiria kumsajili kiungo wao wa zamani wa England aliyekuwa katika timu ya chini ya miaka 21 James Garner, 24, ambaye mkataba wake na Everton unamalizika msimu ujao wa joto. (Mail)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea inamfuatilia beki wa kati wa Ufaransa wa Rennes, Jeremy Jacquet, 20, na mshambuliaji wa Saint-Etienne, Djylian N’Guessan, 17, lakini kipaumbele chao ni kuuza wachezaji akiwemo mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi, 27, na mawinga wa Uingereza Raheem Sterling, 31, na Tyrique George, 19. (Athletic – subscription required)

Soma zaidi:
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Newcastle United, Sandro Tonali, analengwa na Juventus huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kurudi Serie A, huku pia wakimtaka mlinzi wa Tottenham na Romania, Radu Dragusin, ambaye pia anahitajika na Roma. (La Gazzetta dello Sport – in Italian)

Fulham na Crystal Palace wanamfuatilia mchezaji wa Manchester City Oscar Bobb, 22, ikiwa klabu hiyo itaruhusu aondoke Januari – lakini vilabu nje ya Uingereza, ikiwa ni pamoja na Sevilla, pia vinamtaka kiungo huyo wa kati wa Norway. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sporting imewapita wapinzani wao wa Ureno Porto katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa West Ham Luis Guilherme, na wanakaribia kukubaliana kuhusu uhamisho wa kudumu wa mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 19. (ESPN Brazil – in Portuguese)

Tottenham wanataka kuendelea kuwa na beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24 Micky van de Ven kwa kumpa mkataba mpya ulioboreshwa wa muda mrefu. (Athletic – subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool huenda ikafanya uhamisho wa mkopo wa miezi sita kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ureno Goncalo Ramos, 24, kama suluhisho la muda mfupi kwa kukosekana kwa mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 26 aliyejeruhiwa. (Caught Offside)

Wolves wanatazamia kupata dili la kumsajili mchezaji wa zamani wa Bournemouth na Nottingham Forest, Sam Surridge, mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27, ambaye alifunga mabao 24 kwa Nashville wakati wa msimu wa Ligi Kuu ya Soka (MLS) wa 2025. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool bado hawajaamua kama watamruhusu kiungo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18, Trey Nyoni, kuondoka klabuni hapo wakati wa dirisha la uhamisho la Januari, lakini wanafanya mazungumzo na vilabu vya Ligi ya Primia na Ligi ya Mabingwa. (Teamtalk)

Sevilla, Real Oviedo na klabu ya zamani ya Getafe wana nia ya kumrudisha mshambuliaji wa Bournemouth na Uturuki Enes Unal mwenye umri wa miaka 28 nchini Uhispania. (Fichajes – in Spanish).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *