Wataalamu wametilia shaka lengo la Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mashambulizi ya kijeshi nchini Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa kundi la DAESH (ISIS/ISIL) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wataalamu wametaja hujuma hiyo kuwa ya kisiasa zaidi kuliko ya kijeshi. Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kiarabu cha Nigeria, Dkt. Al-Khidr Abdel-Baqi, alithibitisha kwa Sputnik kwamba “maeneo yaliyolengwa si ngome za jadi za ISIS au Boko Haram.”

Amesema huenda kuna “makubaliano ya kificho kati ya Washington na Abuja ya kufanya operesheni ndogo zinazohudumia maslahi ya pande zote mbili.” Abdel-Baqi alionya kuwa “kuendeleza mashambulio kunaweza kuchochea maandamano na kuiweka serikali katika hali ngumu ya kisiasa.” Pia alibainisha kuwa “kulenga maeneo yenye Waislamu wengi karibu na Sokoto kunabeba ishara za kisiasa na kidini.”

Kwa mujibu wa Abdel-Baqi, “Wanigeria wanasubiri siku zijazo kufichua nia na matokeo ya mashambulio hayo.”

Mtaalamu wa siasa kutoka Syria, Dkt. Alaa Al-Asfari, aliambia Sputnik kwamba “Washington inatumia shughuli za makundi yenye misimamo mikali kuendeleza hali ya kutokuwa na utulivu.” Alionya kuwa “mashambulio haya yanaweza kufungua njia ya mipango ya kugawa Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.”

Wataalamu wanakubaliana kwa kauli moja kuwa Marekani ndiyo inayopata faida kubwa zaidi kutokana na kuendelea kwa mgogoro na machafuko nchini Nigeria. Wanigeria wengi wanashangaa ni kwa nini jimbo la Sokoto limelengwa katika hali ambayo ngome za magaidi ni katija jimbo la Borno, Niger, na Kebbi.

Mwezi uliopita, Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza nia yake ya kuishambulia Nigeria kijeshi kwa madai kuwa kuna ukatili mkubwa dhidi ya Wakristo.

Maafisa wa Nigeria wanapinga kutajwa mgogoro wa usalama wa taifa hilo kama mateso ya kidini.

Mamlaka za Nigeria zimesema makundi yenye silaha yanashambulia Waislamu na Wakristo kwa pamoja, na madai ya Marekani kuhusu ukatili wa kimfumo dhidi ya Wakristo yanarahisisha mno mgogoro mgumu unaosababishwa na uhalifu, malalamiko ya ndani na hali ya kutokuwa na utulivu wa muda mrefu.

Mwezi uliopita, Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, alisema taswira ya Nigeria kama taifa lisilo na uvumilivu wa kidini “haiakisi uhalisia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *