
Kazem Jalali, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia amekutana na kufanya mazungumzo na Albir Hazrat Krganov, Mufti wa Moscow na Mwenyekiti wa Baraza la Kiroho la Waislamu wa Russia, na kujadili namna ya kupanua ushirikiano wa kidini.
Katika mazungumzo hayo, Kazem Jalali, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia, na Albir Hazrat Krganov, Mufti wa Moscow na Mwenyekiti wa Baraza la Kiroho la Waislamu wa Russia wawili hao wamesisitiza haja ya ushirikiano kati ya ulimwengu wa Kiislamu na nchi huru dhidi ya sera za udanganyifu na za upande mmoja za Magharibi.
Akizungumzia uungaji mkono wa Magharibi kwa uhalifu wa utawala wa Kizayuni na undumakuwili wao kuhusu haki za binadamu, balozi wa Iran mjini Moscow alisema: “Madola ya Magharibi yanaunga mkono mauaji ya halaiki huko Gaza na Lebanon chini ya kauli mbiu ya haki za binadamu, lakini Iran, Russia na China zinapinga udanganyifu huu na ushirikiano wa pande nyingi utaamua mustakabali wa dunia.”
Katika mkutano huu, Mwenyekiti wa Bunge la Kiroho la Waislamu wa Russia pia alielezea kuridhika kwake na maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na Russia na kuzingatia ushirikiano wa nchi za Kiislamu na Russia chini ya vikwazo kama ishara ya heshima ya Uislamu kwa haki za binadamu.