Chad imelaani shambulio la Vikosi  vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa mpakani kati ya nchi hizo mbili, ambalo limesababisha vifo vya wanajeshi wawili wa Chad.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ndege isiyo na rubani ya Vikosi vya Msaada wa Haraka, ambavyo vinapigana dhidi ya jeshi la Sudan, vilitekeeza shambulio katika mji wa Al-Tina siku ya Ijumaa.

Makao makuu ya jeshi la Chad yameelezea shambulio hilo kama “uchokozi usio na msingi” na kuongeza kuwa yana “haki ya kujibu kwa njia zote za kisheria” iwapo kutatokea ukiukwaji wowote zaidi wa eneo la kitaifa.

Kulingana na afisa wa jeshi la Chad, hii ni mara ya kwanza tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan miaka miwili iliyopita ambapo jeshi la Chad limelengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *