
Kitengo cha Sudan cha Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) kimetangaza siku ya Ijumaa, Desemba 26, 2025, kwamba kilizuru mji wa El-Fasher, ambao ulitekwa Oktoba 26 na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo vimekuwa vikipigana vita na jeshi la Sudan tangu Aprili 15, 2023. Hii ni ziara ya kwanza ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika mji huu magharibi mwa Sudan, ambapo ripoti zinaonyesha mauaji, ukatili wa kingono, na ukatili dhidi ya raia wanaokimbia.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mnamo Desemba 26, 2025, miezi miwili baada ya RSF kuiteka El-Fasher, ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliweza kuzuru mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, mji wa kimkakati nchini Sudan. “Kufuatia mazungumzo marefu ya kibinadamu, ujumbe wa tathmini wa Umoja wa Mataifa umezuru El-Fasher leo,” imesema taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Denise Brown, Mratibu Mkazi na Mratibu wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan. “Huu ni ujumbe wa kwanza uliofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifakatika mji huu baada ya miezi kadhaa ya mapigano makali, kuzingirwa, na ukiukwaji mkubwa dhidi ya raia na wafanyakazi wa kibinadamu. Tangu kuanza kwa vita, mamia ya maelfu ya raia wamelazimika kukimbia El-Fasher na maeneo ya jirani,” taarifa hiyo ilmeongeza, bila kutoa maelezo ya ukaguzi huo.
Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kibinadamu yameomba mara kwa mara ufikiaji wa El-Fasher, ambapo mawasiliano bado hayajakamilika.
Katika mitandao ya kijamii, Massad Boulos, mshauri mkuu wa Marekani kuhusu masuala ya Kiarabu na Afrika, ameelezea kuridhika kwake: “Tunafurahi kuona kuwasili kwa ujumbe wa tathmini wa Umoja wa Mataifa huko El-Fasher, uthibitisho kwamba diplomasia ya Marekani inasaidia kuokoa maisha ya watu. Ufikiaji huu muhimu unafuatia miezi kadhaa ya mazungumzo yaliyoongozwa na Marekani na kazi isiyochoka ya OCHA na washirika wengine wa kibinadamu walio nchini Sudan. Tunatumai kwamba misafara ya misaada itafika El-Fasher mara kwa mara baada ya kuzingirwa huku kwa kutisha.”
Katika ripoti iliyochapishwa katikati ya mwezi Desemba, Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu (HRL) katika Chuo Kikuu cha Yale ilibainisha kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) “viliharibu na kuficha ushahidi wa mauaji ya halaiki yaliyoenea.”
“Ujumbe muhimu, asante kwa timu,” Tom Fletcher, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu na Mratibu wa Dharura wa Msaada amebainisha.
Katika kituo chao ca Telegram kwa Kiarabu, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimekaribisha “ziara ya iliyofanikiwa ya ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) na Idara ya Usalama ya Umoja wa Mataifa (UNDSS) katika jiji la El-Fasher, ambapo ujumbe huo ulitathmini hali ya watu waliohamishwa na mahitaji yao ya kibinadamu, ukajadili kiwango cha huduma walizopewa, na kusikiliza masimulizi ya moja kwa moja kutoka kwa watu waliotoroka makazi yao ambao wako katika kambi.”
RSF ilielezea maeneo yaliyokaguliwa na ujumbe huo. “Wanatangaza utayari wao kamili wa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na mashirika yote ya kimataifa ya kibinadamu ili kurahisisha kazi yao na kuwawezesha kutimiza jukumu lao la kibinadamu katika maeneo ya Darfur na Kordofan.”
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hatari ya ukatili huko Kordofan
Darfur, magharibi mwa Sudan, na Kordofan, ndani zaidi ya bara, inakumbwa na mapigano makali kwa miezi kadhaa kati ya wanamgambo wa Jenerali Hemedti na jeshi la Jenerali al-Burhan, ambao wamekuwa vitani tangu Aprili 15, 2023. Mgogoro huu umegharimu maisha ya maelfu ya watu, mamilioni ya watu wakiwa wamekimbia makazi yao, na kusababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.