
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kukiukaji wazi mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Somalia.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baghai amesema, hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kukiuka pakubwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Somalia kwa kujaribu kuendeleza njama ya kuisambaratisha nchi hiyo ya Kiislamu ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimsingi za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, akisisitiza msimamo wa kimsingi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu umuhimu wa kuhifadhi uhuru wa kitaifa, umoja wa ardhi ardhi wa eneo la Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, alielezea hatua hii mbaya ya utawala wa Kizayuni kama inayoendana na sera ya utawala huo ghasibu ya kuyumbisha nchi za eneo hilo na kuongeza ukosefu wa usalama katika eneo la Bahari Nyekundu na Pembe ya Afrika. Huku akiunga mkono msimamo thabiti wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Umoja wa Afrika katika kulaani kitendo cha utawala wa Kizayuni, Ismail Baghaei ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti na jamii ya kimataifa ili kukabiliana na kitendo hiki cha kujitanua na kutishia cha utawala huo vamizi.