Rais wa Urusi Vladimir Putin akiongoza mkutano wa wafanyabiashara wakubwa huko Kremlin huko Moscow mnamo Februari 24, 2022.

Chanzo cha picha, ALEXEY NIKOLSKY/SPUTNIK/AFP

    • Author, Vitaly Shevchenko
    • Nafasi, Mhariri wa BBC Monitoring Urusi
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Idadi ya mabilionea nchini Urusi imefikia kiwango cha juu sana hasa wakati wa vita vya Ukraine. Lakini katika kipindi cha miaka 25 Vladimir Putin amekuwa madarakani, matajiri na wenye nguvu wa Urusi – wanaojulikana kama oligarchs – wamepoteza karibu ushawishi wao wote wa kisiasa.

Hii ni habari njema kwa rais wa Urusi. Vikwazo vya Magharibi vimeshindwa kuwageuza matajiri hao kuwa wapinzani wake, na sera zake za pata pote zimewageuza kuwa wafuasi wa kimya.

Bilionea wa zamani wa Oleg Tinkov aliyeongoza sektabya benki anajua jinsi sera hiyo inavyofanya kazi.

Siku moja baada ya kuwaita wanaoendeleza vita vya Ukraine kama “vichaa” katika chapisho la Instagram, Kremlin iliwasiliana na watendaji wake. Waliambiwa Benki yake ya Tinkoff, ambayo ilikuwa ya pili kwa ukubwa nchini Urusi wakati huo, ingetaifishwa endapo haitakatiza mahusiano na mwanzilishi wake.

“Sikuwa huru kujadili bei,” Tinkov aliambia New York Times. “Nilikuwa kama mateka – unachukua kile unachopewa. Sikuwa na uwezo wa kujadili chochote.”

Ndani ya wiki moja, kampuni inayohusishwa na Vladimir Potanin – mfanyabiashara wa tano kwa utajiri nchini Urusi, ambaye hutoa nickel kwa injini za ndege za kivita – ilitangaza kuwa inanunua benki hiyo. Iliuzwa kwa 3% tu ya thamani yake halisi, anasema Tinkov.

Mwishowe, Tinkov alipoteza karibu dola bilioni tisa za Kimareni ($9bn) ya utajiri aliokuwa nao hapo awali, na kuondoka Urusi.

Mwanamume aliyevaa kofia nyeupe ya baseball na fulana ya kijivu anatabasamu akiwa amesimama chini ya mti

Chanzo cha picha, Chris Graythen/Getty Images

Hii ni mbali na jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya Putin kuwa rais.

Katika miaka iliyofuata baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti, baadhi ya Warusi walitajirika sana kwa kumiliki makampuni makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali, na kwa kutumia fursa za ubepari changa wa nchi yao.

Utajiri wao mpya uliwaletea ushawishi na mamlaka wakati wa machafuko ya kisiasa na kuwafanya wakajulikane kama kama wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa.

Oligarch mwenye nguvu zaidi wa Urusi, Boris Berezovsky, alidai kuwa ndiye aliyemsaidua Putin kuwa rais mnamo 2000, na miaka kadhaa baadaye aliomba msamaha kwa kufanya hivyo: “Sikuona udhalimu wake kama mtu mwenye pupa na mnyang’anyi, mtu ambaye angeminya uhuru na kurudisha nyuma maendeleo ya Urusi,” aliandika mnamo 2012.

Berezovsky huenda kuwa alizidisha jukumu lake, lakini mabwenyenye wa Urusi bila shaka walikuwa na uwezo kushinikiza mabadiliko katika uongozi wa ngazi ya juu nchini.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuomba msamaha, Berezovsky alipatikana amekufa katika mazingira ya kutatanisha akiwa uhamishoni nchini Uingereza. Kufikia wakati huo, ushawishi wa matajiri wa Urusi umedidimia.


Mwanamume aliyevaa nguo nyeusi anasimama kwenye ngazi mbele ya nyumba nzuri

Chanzo cha picha, Hulton Archive/Getty Images

Kutokana na hilo wakati Putin alipokusanya matajiri wa Urusi katika Kremlin saa kadhaa baada ya kuamuru uvamizi kamili wa Ukraine mnamo 24 Februari 2022, hawakuwa na uwezo wa kupinga lolote, ingawa walifahamu changamoto inayowakabili

“Natumai katika mazingira haya mapya, tutafanya kazi pamoja kwa ufanisi,” aliwaambia.

Mwanahabari mmoja aliyekuwepo kwenye mkutano huo aliwataja mabilionea waliokusanyika kuwa watu “waliojawa na hofu na kukosa usingizi”.

Maandalizi ya uvamizi huo yalikuwa mabaya sana kwa mabilionea wa Urusi, matokeo yake yalionekana mara moja.

Kulingana na jarida la Forbes, katika mwaka hadi Aprili 2022, idadi yao ilishuka kutoka 117 hadi 83 kwa sababu ya vita, vikwazo na kuporomoka kwa thamani ya ruble (sarafu ya Urusi). Kwa pamoja, walipoteza takribani dola bilioni 263 – au 27% ya utajiri wao kila mmoja kwa wastani.

Matumizi makubwa ya fedha katika vita yalichochea ukuaji wa uchumi wa zaidi ya 4% kwa mwaka nchini Urusi mwaka wa 2023 na 2024. Ilikuwa nzuri kwa baadhi ya matajiri wakubwa wa Urusi ambao hawakuwa wakitengeneza mabilioni moja kwa moja kutokana na kandarasi za ulinzi.

Mnamo mwaka wa 2024, zaidi ya nusu ya mabilionea wa Urusi walikua na jukumu maalum katika kusambazaji wa vifaa vya jeshi au walinufaika na uvamizi huo, anasema Giacomo Tognini, kutoka timu ya Forbes inayotathmini Utajiri wa watu.

“Hiyo haijumuishi matajiri ambao hawahusiki moja kwa moja, lakini wanahitaji uhusiano wa aina fulani na Kremlin. Na nadhani ni sawa kusema kwamba mtu yeyote anayeendesha biashara nchini Urusi anahitaji kuwa na uhusiano na serikali,” aliiambia BBC.

Mwaka huu ilishuhudia idadi kubwa zaidi ya mabilionea nchini Urusi – 140 – kwenye orodha ya Forbes. Thamani yao ya pamoja ($580bn) ilikuwa tu $3bn aibu ya juu wakati wote kusajiliwa katika mwaka kabla ya uvamizi.

Huku akiwaruhusu waaminifu kupata faida, Putin ameendelea kuwaadhibu wale ambao wamekataa kufuata mkondo huo.

Warusi wanakumbuka vizuri sana kile kilichotokea kwa tajiri wa mafuta Mikhail Khodorkovsky. Aliyekuwa tajiri zaidi nchini Urusi, alizuiliwa jela miaka 10 baada ya kuanzisha shirika la kutetea demokrasia mwaka 2001.

Mtu tajiri zaidi wa Urusi na mfanyabiashara mkubwa wa mafuta Mikhail Khodorkovsky akiwa katika gereza la "Matroska tishina" kwenye skrini ya runinga wakati wa kiunga cha video katika mahakama ya Moscow, 15 Januari 2003.

Chanzo cha picha, AFP

Tangu uvamizi huo, karibu matajiri wote wa Urusi wamesalia kimya, na wale wachache waliopinga hadharani hatua ya Putin kuivamia Ukraine wamelazimika kuitoroka nchi yao na utajiri wao mwingi.

Matajiri zaidi wa Urusi ni muhimu kwa juhudi za vita za Putin, na wengi wao, wakiwemo wafanyabiashara 37 walioitwa Kremlin mnamo 24 Februari 2022, waliwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.

Lakini juhudi za nchi za Magharibi za kuwalemaza kiuchumi ili kuwashinikiza wabadili misimamo yao dhidi ya Kremlin, zimegonga mwamba, kwani mabilionea hao wameamua kufanya kazi pamoja kulinda mali zao.

Nchi za Magharibi zilikurupuka “Hakukuwa na mpango kamili, hakuka na wazo wala mpango wowote ambao ungemshawishi yeyote kati yao kuiasi Urusi. Mali zilizuiliwa, akaunti kufungwa, mali kuchukuliwa,”anasema Alexander Kolyandr wa Kituo cha Uchambuzi wa Sera za Ulaya (CEPA).

Yote hayo yalimsaidia Putin kuwaleta pamojs mabilionea, mali zao na pesa zao, na kuzitumia kusaidia uchumi wa vita vya Urusi,” anaiambia BBC.

Kuondoka kwa makampuni ya kigeni baada ya uvamizi wa Ukraine kuliacha ombwe lililojazwa haraka na wafanyabiashara walio na uhusiano wa karibu na Kremlin ambao waliruhusiwa kununua mali yenye faida kubwa kwa bei nafuu.

Hatua hii iliunda “jeshi jipya la watiifu wenye ushawishi na kazi”, anasema Alexandra Prokopenko wa Kituo cha Carnegie Russia Eurasia.

“Ustawi wao wa siku zijazo unategemea kuendelea kwa makabiliano kati ya Urusi na nchi za Magharibi,” wakati hofu yao kubwa ikiwa ni kurejea kwa mmiliki wa awali, anasema.

Mwaka 2024 mabilionea wapya 11 waliibuka nchini Urusi kwa njia hiyo, kulingana na Giacomo Tognini.

Rais Putin wa Urusi amedumisha mshikamano thabiti kwa wahamasishaji wakuu wa nchi hiyo, licha ya vita na vikwazo vya Magharibi – na kwa namna moja au nyingine kwa ajili ya maslahi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *