
Upigaji kura unafanyika katika mazingira yenye vikwazo vingi, huku vyama vikuu vya upinzani vikiwa vimepigwa marufuku na raia wakiripoti kutishwa na wanajeshi ili washiriki.
Jenerali Min Aung Hlaing, ambaye aliongoza mapinduzi ya 2021, anatarajiwa kuchukua urais baada ya duru tatu za upigaji kura kukamilika Januari.
Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa mustakabali wa Myanmar lazima uamuliwe kupitia mchakato huru, wa haki, jumuishi na wenye kuaminika unaoakisi matakwa ya wananchi.