
Touadéra, amekuwa madarakani tangu tangu 2016, na amegombea tena baada ya kura ya maoni yenye utata ya 2023 kumruhusu kuongeza mihula.
Mbali na uchaguzi wa rais, pia kuna uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa. Baadhi ya vyama vya upinzani vimetoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi huu.
Touadéra anategemea sana wanajeshi na mamluki wa Urusi, ambao pia wanatuhumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Licha ya utajiri wa almasi na dhahabu, nchi hiyo bado ni maskini sana, na serikali inadhibiti maeneo machache nje ya mji mkuu, Bangui.
Uchaguzi unafanyika wakati nchi ikiwa bado kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza 2013, ingawa vikosi vya kimataifa na msaada wa Urusi na Rwanda vimeleta utulivu kiasi. Hata hivyo, waasi bado wanafanya mashambulizi hasa mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini.