
Rais wa zamani wa Baraza la Seneti Richard nchini Madagascar, Ravalomanana anakabiliwa na utaratibu kisheria. Kiongozi huyu maarufu wa utawala wa Rajoelina, aliyetukanwa na waandamanaji wakati wa maandamano ya hivi karibuni ya Gen Z, alikamatwa siku ya Jumamosi, Desemba 27, nyumbani kwake Antananarivo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry
Richard Ravalomanana alikataa katika siku za hivi karibuni kuripoti mbele ya ofisi ya polisi baada ya kupewa hati ya kuitika. Wachunguzi wanaangazia jukumu alilochukua katika ukandamizaji wa maandamano ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.
Richard Ravalomanana aliongoza “vitendo vya vurugu kukandamiza raia,” alisema Mwanasheria Mkuu katika Mahakama ya Rufaa ya Antananarivo, Didier Alban Razafidralambo, siku ya Jumamosi hii, Desemba 27,mbele ya vyombo kadhaa vya habari vya Madagascar.
Mwanasheria huyo alionyesha kwamba rais wa zamani wa Baraza la Seneti anaweza kushtakiwa kwa “kuhatarisha usalama wa taifa, kuchochea chuki, na kushiriki katika mauaji na kujeruhi watu kwa makusudi.”
Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu 22 waliuawa na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa wakati wa maandamano yaliyosababisha kupinduliwa kwa Rais Andry Rajoelina na kundi la wanajeshi mnamo Oktoba 14.
Kiongozi muhimu katika utawala ulioondolewa madarakani, Richard Ravalomanana akawa kitovu cha hasira za waandamanaji, ambao walimwona kama ishara ya mamlaka ya kimabavu. Siku tatu kabla ya kukamatwa kwake, Mahakama Kuu ya Katiba ilimwondoa katika nafasi yake kama seneta baada ya kubaini kutokuwepo kwake katika mijadala yote kuhusu bajeti ya mwaka 2026.