
Zelenskiy amesema mpango huo unaweza kuwa msingi wa makubaliano ya baadaye ya kumaliza vita na Urusi.
Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo ya kurekebisha rasimu ya awali yenye vipengele 28 — ambayo ilionekana kuunga mkono madai mengi ya Urusi, Zelenskiy alisema wiki hii kwamba misimamo mingi imekaribiana kwa kiasi kikubwa.
Ukraine na Marekani bado hazijafikia mwafaka juu ya masuala mawili makuu: udhibiti wa maeneo ya ardhi na udhibiti wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia — lakini Zelenskiy amesema anatumai kuyajadili yote mawili na Trump.