
Akizungumza katika kikao cha dharura cha Bunge mjini Mogadishu, Mahamud amekosoa tangazo la juzi Ijumaa la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiitaja hatua hiyo kama shambulio la wazi dhidi ya mamlaka, uhuru, umoja wa eneo na watu wa Jamhuri ya Somalia.
Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka Somalia mwaka 1991 na kwa miongo kadhaa imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa. Ingawa inajiendesha kama jamhuri huru yenye sarafu, pasi na jeshi lake, imeendelea kutengwa kidiplomasia tangu ilipotangaza kujitenga.