Kamati ya bonde la maji pangani imeridhishwa na hali ya utunzaji wa bwawa la nyumba ya mungu baada ya wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na masoko kuzunguka bwawa hilo ambalo ni chanzo kikubwa za maji yanayotumika kwenye shughuli za kilimo,uvuvi na uzalishaji wa umeme.