Kufuatia mauaji ya mkazi wa Mtaa wa Zavala Kata ya Buyuni wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Salehe Idd Salehe mnamo Disemba 4, 2024 Jeshi la polisi limetakiwa kutumia uwezo na utaalamu ilionao kuwabaini na kuwakamata waliofanya mauaji hayo yanayohusishwa na kisasi.
Akizungumza katika Mkutano na wananchi wa kata ya Buyuni, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amelitaka jeshi hilo kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala kuhakikisha wahalifu wanatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani.
Inadaiwa kuwa mauaji ya Salehe Idd Salehe aliyekuwa mkazi wa miaka mingi katika kata hiyo unatokana na kupigania kutouzwa kwa maeneo ya wazi ya serikali yakiwemo ya shule, masoko na vituo vya afya na kundi la wahalifu kupitia programu iliyokuwa ikifahamika kwa jina la โViwanja Elfu 20 Kata ya Buyuniโ kati ya mwaka 2003 hadi 2005.
โKamanda RPC wa Ilala nakuagiza, jeshi lako lina mfumo na nyenzo imara sana za uchunguzi na ukamataji, tumia vyombo vyako na utaalamu wako na wakamateni wote waliofanya mauaji haya kwa kuwa inaelekea wanao mtandao mkubwa wa kiuhalifu katika eneo letu la wilaya za kipolisi za Chanika na Ukonga,โ amesema Mpogolo.
Katika hatua nyingine DC Mpogolo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji kupitia Idara ya Mipango Jiji kuyatambua na kuyarejesha maeneo yote wazi ya huduma za jamii yaliyolipiwa na kutengwa na serikali.