Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon ya Hizbullah amesema: “leo, Lebanon iko katikati ya dhoruba na mvurugiko wa utulivu kutokana na sera za Marekani na adui wa Kizayuni.”

Sheikh Naim Qassem, ameyasema hayo alipohutubia katika hauli ya mwaka wa pili ya Hajj Muhammad Hassan Yaghi, mwanachama mwandamizi wa Hizbullah, na akabainisha kwamba njia inayofuatwa na Hizbullah inatoa mwanga wa nuru kwa sababu harakati hiyo ya Muqawama haijaikomboa kusini mwa Lebanon pekee bali imeikomboa Lebanon yote.

Amesema: Hizbullah inazingatia usawa katika kuamiliana na serikali na wananchi na iko wazi kabisa juu ya suala hilo; na kwamba harakati hiyo daima imekuwa ikitoa mchango wa kujenga katika ustawishaji wa nchi na kufanya kazi kulingana na misingi ya sheria.

Sheikh Naim Qassem amebainisha: “tunakabiliwa na mabadiliko ya kihistoria, ya ima kusimamiwa na madola ya kigeni au kuwa huru”, akaongezea kwa kusema: “lazima turejeshe mamlaka ya kujitawala ya Lebanon kwa kumtimua mvamizi”.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah ameeleza kwamba, suala la kuupokonya silaha Muqawama ni njama ya utawala wa kizayuni wa Israel; na kwamba kuupokonya silaha Muqawama ni sehemu ya mradi wa kuangamiza nguvu za Lebanon na njama ya kukiuka mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo katika ngazi zote…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *