Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, NUP, Robert Kyagulani maarufu kama Bobi Wine, sasa anamtaka mgombea wa NRM, rais Yoweri Museveni, kuwataka wafuasi wake kulinda kura zake, badala ya kuagiza waondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Bobi Wine ametoa changamoto hii, ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu mkuu wa majeshi ya nchi hiyo ambaye ni mtoto wa rais Museveni, Muhoozi Kainerugaba, kudai kuwa jeshi halitaruhusu raia kukaa karibu na vituo baada ya kupiga kura, akiwataka waende nyumbani.
Kufuatia tangazo hilo, Bob Wine amemtuhumu rais Museveni kutumia jeshi kuingilia mchakato wa uchaguzi, akisema sheria ya uchaguzi inaruhusu raia kukaa umbali fulani toka kwenye kituo alichopiga kura kushuhudia zoezi la kuzihesabu linavyoendelea.

Bobi Wine amewataka wagombea wenzake wamuunge mkono katika wito wake, wakati huu kukiwa na wasiwasi wa zoezi hilo kugubikwa na udanganyifu pamoja na vitisho toka kwa vyombo vya usalama, ambavyo tangu kampeni zianze, vimekuwa vikidhibiti mikutano ya wanasiasa wa upinzani na hasa ile ya Robert Kyagulani.
Haya yanajiri wakati huu waangalizi wa ndani na nje, wakionesha hofu ikiwa uchaguzi wa mwakani utakuwa huru na haki.