China inafanya mazoezi ya kijeshi kuzunguka Taiwan ikiiga kukamatwa na kuzingirwa kwa maeneo muhimu ya kisiwa hicho, kama onyo dhidi ya “vikosi vya Taiwan.”

Jeshi la ardhini, jeshi la wanamaji, jeshi la anga na kikosi cha roketi vimetumwa kwa ajili ya mazoezi hayo ambayo yanajumuisha mazoezi ya kufyatua risasi za moto, limesema jeshi la China.

Mazoezi hayo yanafanyika siku chache baada ya Marekani kutangaza kuuza silaha kwa Taiwan zenye thamani ya dola bilioni 11 (pauni bilioni 8.2). Hatua hiyo imesababisha upinzani mkali kutoka Beijing ambayo imewekea vikwazo makampuni ya ulinzi ya Marekani.

Taiwan kuongeza ulinzi wake mwaka huu pia kumeikasirisha Beijing, ambayo inadai kisiwa hicho kinachojitawala ni eneo lake.

Ofisi ya rais ya Taiwan imekosoa mazoezi ya China, ikiyaita ni tatizo kwa kanuni za kimataifa.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema imegundua ndege na meli za China zikizunguka Taiwan Jumatatu asubuhi, na wameweka vikosi vyao na mifumo ya makombora tayari ili kufuatilia hali hiyo.

Vikosi viko “tayari” kuilinda Taiwan na “kuwalinda watu wetu”, wizara hiyo imesema.

Ingawa mazoezi ya awali yameanza, jeshi la China lilisema litafanya mazoezi makubwa kuanzia Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *