
Makabiliano hayo yameibuka siku mbili baada ya msikiti wa Alawi ulioko kwenye mji wa Homs kushambuliwa kwa bomu na kuwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine 18 wakati wakifanya ibada na kusababisha maelfu ya waandamanaji kukusanyika kwenye miji ya pwani ya Latakia, Tortus na mingine.
Maafisa wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha vilipuzi viliwekwa ndani ya msikiti huo, lakini bado mamlaka hazijamtambua mshambuliaji.
Syria imekabiliwa na mawimbi kadhaa ya mapigano ya kidini tangu kuangushwa kwa utawala wa Bashar al Assad Disemba 2024, na kuhitimisha karibu miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.