Serikali imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bwawa la maji la Mwambazi mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, kwa lengo la kukabiliana na uhaba wa maji unaowakabili wakazi wa mji huo ambao nyakati za kiangazi hulazimika kutumia mgao kutokana na vyanzo vilivyopo kushindwa kukidhi mahitaji.
Bwawa hilo, linalojengwa pembezoni mwa msitu wa hifadhi wa Mbizi, linatarajiwa kuwa suluhisho la upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya mji yanayoendelea kujengwa kwa kasi lakini yakikosa huduma ya maji kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Taka Mjini Sumbawanga (SUWASA).
✍Sammy Kisika
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates