Watoa huduma za afya mkoani Mtwara wametakiwa kujipanga ili kuboresha utoaji wa huduma katika vituo vyao na kuwa vivutio kwa wagonjwa, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa fedha kutoka Mfuko wa Bima za Afya kwa Wote (CHF) zilizoboreshwa.
Mpango huu unalenga kuhakikisha jamii zenye hali za chini zinapata huduma kwa wakati unaofaa, tofauti na awali ambapo malipo yalitegemea huduma iliyotolewa, hivyo kurahisisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote.
✍John Kasembe
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates