Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba leo Desemba 29, 2025 amekagua hali za uzalishaji na usambazaji wa maji eneo la Ruvu Chini, mkoani Pwani.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Dkt Mwigulu amesema ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji unaotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Serikali ilianza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
“Mipango hii ya ujenzi wa miradi inayolenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji ilianza muda mrefu, Serikali iliona na ilianza kutafuta majawabu ya hali hii miaka mitatu iliyopita kwa kujenga miradi mikubwa itakayotoa matokeo chanya”.