XC

Chanzo cha picha, EPA

Rais
Volodymyr Zelensky amekanusha madai ya Urusi kwamba Ukraine imefanya shambulio
la ndege zisizo na rubani kwenye moja ya makazi ya Rais Vladimir Putin, na
kuishutumu Moscow kwa kujaribu kuvuruga mazungumzo ya amani.

Waziri wa
Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anadai Kyiv ilifanya shambulio usiku kwa
kutumia ndege 91 zisizo na rubani (UAVs) kwenye makazi ya Putin katika eneo la
kaskazini magharibi mwa Novgorod nchini Urusi.

Urusi imesema
sasa itapitia upya msimamo wake katika mazungumzo ya amani. Bado haijabainika
Putin alikuwa wapi wakati wa shambulio hilo.

Zelensky amekanusha
madai hayo akisema ni “uongo wa Urusi,” uliokusudiwa kuipa Kremlin
kisingizio cha kuendelea na mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Amesema Urusi
imewahi kushambulia majengo ya serikali huko Kyiv.

Zelensky alisema
kwenye X: “Ni muhimu dunia isikae kimya sasa. Hatuwezi kuruhusu Urusi
kudhoofisha juhudi za kufikia amani ya kudumu.”

Katika
taarifa aliyoichapisha kwenye Telegram siku ya Jumatatu, Lavrov alisema ndege
zote zisizo na rubani 91 alizodai zilirushwa kuelekea nyumbani kwa Putin
zilizuiliwa na kuharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi.

Aliongeza
kuwa hakukuwa na ripoti za majeruhi au uharibifu kutokana na shambulio hilo.

“Kwa kuongezeka
jinai za utawala wa Kyiv, ambao umebadilika na kuwa na sera ya ugaidi wa
serikali, msimamo wa Urusi katika mazungumzo wa kusaka amani utapitiwa upya,”
alisema.

Lakini
aliongeza kwamba Urusi hana na nia ya kujiondoa katika mchakato wa mazungumzo
na Marekani, shirika la habari la Urusi Tass liliripoti.

Madai hayo
ya Moscow yanakuja baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Ukraine huko Florida
siku ya Jumapili, ambapo Marais Trump na Zelensky walijadili mpango mpya wa
amani wa kukomesha vita.

Baada ya
mkutano huo, Zelensky aliambia Fox News Jumatatu kwamba kuna “uwezekano wa
kumaliza vita hivi” mwaka 2026.

Lakini
alisema Ukraine haiwezi kushinda vita bila msaada wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *