
Wakimbizi wa Mali wanaendelea kuwasili kusini-mashariki mwa Mauritania. Kulingana na Shirika la Umoja a Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR, zaidi ya watu 1,100 walivuka mpaka wiki iliyopita, na hivyo kuongeza idadi ya wakimbizi wapya tangu mwisho wa mwezi Oktoba hadi takriban 7,300.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wimbi hili linaongeza idadi ya wakimbizi wa Mali zaidi ya 300,000 ambao tayari wako nchini, athari ya mgogoro wa usalama ambao umedumu kwa zaidi ya miaka kumi na umezidi kuwa mbaya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Raia hawa wanaokimbia makundi yote mawili yenye silaha ya wanajihadi nchini Mali na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Mali, linaloungwa mkono na wanamgambo wa Urusi, wanawasili wakiwa katika hali mbaya zaidi, na masirika yanayotoa misaada ya kibinadamu yana hofu kwamba hali hi ya watu kutoroka Mali itaendelea. Katika wiki za hivi karibuni, raia wengi wa Mali walitoroka makazi yao.
Huko Léré, katika jimbo la Timbuktu, kizuizi kilichowekwa na wanajihadi wa JNIM kinaendelea. Ukosefu wa usalama, pamoja na kupanda kwa bei ya bidhaa za msingi, kunawalazimisha wakazi kukimbia. Ili kufikia nchi jirani ya Mauritania, baadhi wanasafiri zaidi ya kilomita 70 kwa miguu. Miongoni mwao ni wanawake na watoto wengi, na idadi inayoongezeka ya wazee.
Wadau wa masuala ya kibinadamu sasa wana hofu ya kuongezeka zaidi kwa mgogoro huu ikiwa utulivu katika hali ya usalama utaruhusu raia wengi zaidi kuondoka katika maeneo yaliyotengwa kwa sasa. Hivi ndivyo Carole Lalève, Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi(UNHCR) nchini Mauritania, anavyoelezea.
“Sioni uwezekano wowote wa utulivu wa haraka kwa vurugu hizi kwa sasa.” Kinachotia wasiwasi ni kwamba mzozo upande wa pili wa mpaka unaonekana kuenea hadi maeneo ya kati zaidi ya Mali, jambo la hivi karibuni ambalo linaweza kusababisha wimbi zaidi la wakimbizi. Ndiyo maana, pamoja na serikali na washirika wetu, tunaandaa, hata kwa rasilimali zetu chache, mpango wa dharura.
Wanapowasili, maelfu ya wakimbizi hupewa hifadhi katika kambi kubwa, kama ile ya Mbera, ambapo hali ya maisha ni ngumu sana. Maji na makazi ni machache. Wengi pia huchagua kuishi katika vijiji vilivyo karibu, jambo ambalo linachanganya utambuzi na usajili wa wakimbizi wapya. Kulingana na mamlaka za eneo hilo na mashirika ya kibinadamu, karibu nusu ya wakazi wa eneo la Hodh Chargui nchini Mauritania sasa wana asili ya Mali.