Wenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu, timu ya taifa ya Morocco, imejikatia tiketi ya kucheza hatua ya kumi na sita bora baada ya kupata ushindi dhidi ya Zambia ambayo imeaga rasmi mashindano.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Morocco imefuzu hatua hii baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Zambia, shukrani kwa magoli ya El Kaabi Ayoub na Brahimi Diaz.

Mbali na Morocco, timu nyingine kutoka kundi A inayoungana na Morocco ni Mali ambayo ilitoka sare ya bila kufungana na Comoro.

Aidha mabingwa mara nyingi zaidi wa michuano hii, timu ya taifa ya Misri, nayo ilifuzu hatua ya mtoano toka kundi B licha ya sare ya kutofungana na Angola, sasa ikiungana na Afrika Kusini, iliyopata ushindi wa goli 3 kwa 2 dhidi ya Zimbabwe.

Morocco imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 ya mashindano ya Afcon 2025.
Morocco imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 ya mashindano ya Afcon 2025. AP – Themba Hadebe

Mechi nyingine za kukamilisha hatua ya makundi zitachezwa hivi leo ambapo katika kundi C Nigeria watacheza na Uganda, huku Tanzania wakiwakaribisha Tanzania, Nigeria na Tunisia zikihitaji ushindi ama sare yoyote kufuzu hatua ya mtoano.

Mechi nyingine ni zile za Kundi D, ambapo Benin Watacheza na Senegal, wakati DRC watachuana na Botswana, mechi ambazo DRC, Senegal na Benin zitahitaji ushindi ili kupata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *