Zaidi ya wahamiaji elfu 3 walipoteza maisha mwaka huu wakati wakijaribu kuingia Uhispania,hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika linalotetea haki za wahamiaji la Hispania, idadi hii ikiwa ni pungufu na ile iliyotolewa mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika lisilo la serikali la Caminando Fronteras zaidi ya wahamiaji 3,090 walikufa maji kati ya Januari na katikati ya Desemba mwaka huu, wakiwemo wanawake 192 na watoto 437.

Nayo ripoti ya Wizara ya mambo ya ndani ya Uhispania ikionyesha   takriban wahamiaji 36,000 waliingia nchini humo  kwa njia ya bahari na nchi kavu wakati huo, kutoka zaidi ya 60,000 mwaka uliopita, wengi wakitoka taifa la Mauritania.

Aidha ripoti imeonesha idadi kubwa ya wahamiaji wanatoka nchi za Somalia, Sudan, Sudan Kusini na Senegal.

Mwaka uliopita Mauritania ilitia saini mkataba wa uhamiaji wa Euro milioni 210 na Umoja wa Ulaya  ili kukabliana na wahamiaji haramu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *