Marekani imezindua mpango wa kutafuta Dola Bilioni 2 kusaidia kuinua mfuko maalum unaoshughulikia masuala ya kibinadamu katika nchi mbalimbali zinazokabiliana na utovu wa usalama.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja, baada ya Marekani, kupitia Wizara ya Mambo ya nje, kutoa Dola Bilioni 2 kuimarisha mfuko huo ili kusaidia operesheni za kutoa misaada ya kibinadamu mwaka 2026.

Tom Fletcher, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia maswala ya kibinadamu OCHA, amesema fedha hizo zitawasaidia watu wanaoteseka kwa sababu ya vita, katika nchi 17.

Mamilioni ya Wakongomani, ni baadhi ya watu wanaotarajiwa kunufaika na misaada ya kibinadamu, kutokana na vita Mashariki mwa nchi hiyo kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23/AFC.

Kuelekea mwaka 2026, Umoja wa Mataifa ulikuwa umepanga bajeti ya Dola Bilioni 2.5 kusaidia kushughulikia changamoto za kibinadamu Mashariki mwa DRC, lakini mfuko huo, haujakuwa ukipokea mchango unaohitajika, huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *