
Nchi ya Saudi Arabia, inaishtumu Falme ya Kiarabu, kwa kuhusika kwenye vitendo inavyosema ni hatari nchini Yemen.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kauli hii imekuja, baada ya waasi wanaoungwa mkono na Saudi Arabia nchini Yemen, kushambulia meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha katika bandari ya Mukalla , iliyokuwa inakwenda katika nchi ya Falme ya Kiarabu.
Kutokana na hatua hiyo, uongozi wa Yemen umetangaza kusitisha mkataba wa kiusalama na Falme za Kiarabu.
Vikosi vya Falme za Kiarabu nchini Yemen, vimetakiwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 24 zijazo, na kutangaza kufungwa kwa mipaka ya angaa, ardhi na bahari.
Katika wiki za hivi karibuni, waasi wanaoungwa mkono na Falme za Kiarabu, wamekuwa wakijaribu kuanzisha upya jimbo lililokuwa linajitegemea Kusini mwa Yemen.