‎#HABARI: Abiria wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Dodoma kupitia Reli ya Kisasa (SGR), wamepongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuchukua hatua za haraka kushughulikia changamoto za usafiri zilizojitokeza na kurejesha huduma kama kawaida.

‎Wakizungumza baada ya TRC kuomba radhi kufuatia usumbufu wa safari uliotokea, abiria hao wakiwemo Wafanyabiashara na wajasiriamali wameeleza kuridhishwa na namna shirika hilo lilivyoshughulikia tatizo hilo kwa muda mfupi.

‎Awali, TRC ilitoa taarifa ya kuomba radhi kwa abiria wake kutokana na usumbufu uliosababishwa na changamoto za nishati kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini, ambapo kupitia taarifa hiyo, shirika hilo liliahidi kuendelea kuboresha huduma zake, kushughulikia changamoto kwa wakati, pamoja na kuongeza safari za ziada kati ya Dar es Salaam na Dodoma ili kuendeleza shughuli za kiuchumi na kijamii nchini.


‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *