Serikali imesema kuwa kuanzia sasa, wawekezaji watahusika moja kwa moja katika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uwekezaji kabla ya kuanza shughuli zao za uzalishaji, ikiwa ni moja ya njia za kupunguza malalamiko ya muda mrefu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, amesema hayo mkoani Pwani wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya uwekezaji na uzinduzi wa taarifa ya hali ya uwekezaji kwa mwaka 2025.

#AzamTVUpdates
✍️ Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *