Timu ya Taifa ya Tanzania imefuzu kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya AFCON 2025 baada ya kutoka na sare ya bao 1 – 1 dhidi ya Tunisia usiku wa leo katika uwanja wa “Stade Olympique Annexe Complexe Sportif Prince Abdellah” nchini Morocco.

Stars imefuzu kutinga hatua ya 16 bora kupitia mlango wa “best looser” baada ya kumaliza nafasi ya tatu ya kundi C wakiwa na Alama 2 nyuma ya Tunisia wenye alama 4 na Vinara Nigeria wakiwa na alama 9 huku Uganda akiburuza mkia kwenye kundi hilo na alama yake 1.

Ikumbukwe kwamba Bingwa mtetezi wa taji hili @elephantdecotedivoire na mwana nusu fainali @beninfootball walipitia mlango wa “best looser” katika michuano hiyo msimu jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *