Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Mkoani Tanga Reuben Kwagilwa anatarajiwa kufunga rasmi mashindano ya “Moja kw amoja Cup” yaliyohusisha timu 12 kutoka kata mbalimbali za jimbo hilo, ambapo mashindano hayo yamedumu kwa miezi mitatu huku na jumla ya timu 14 zimeshiriki.

Lengo kuu la mashindano hayo ni kuhamasisha umuhimu wa amani, mshikamano na uwajibikaji wa vijana katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo katika kata zao.

Mashindano hayo yanaratibiwa na kusimamiwa na Diwani wa Kata ya Chanika kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Handeni.

Kwa upande wa zawadi, mshindi wa kwanza anatarajiwa kupata kiasi cha shilingi 500,000/=, mshindi wa pili shilingi 200,000/= pamoja na zawadi nyingine kwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano hayo.

Ligi hiyo inatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 01 Januari 2026, sambamba na mapokezi ya Mwaka Mpya, katika Uwanja wa Kigoda
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *