Dunia imeanza sherehe za kuuaga mwaka 2025 uliogubikiwa na mambo lukuki ikiwemo ushuru wa Rais Trump, usitishaji wa mapigano huko Gaza, pamoja na mazungumzo ya kusaka amani kuhusu vita vya Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kando na ushuru wa Rais na makubaliano ya kusitisha vita mashariki ya kati, nchi za Ulaya zilikabiliwa na majanga mbalimbali ikiwemo moto wa misitu, baadhi ya mataifa ya Afrika nayo yakiripoti ukame na hata mafuriko.

Nchi za kusini mashariki mwa Asia zilikabiliwa na mvua kubwa iliyosababisha maafa, huku nchi zengine za dunia zikishuhudia baridi zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa miaka iliotangulia.

Aidha mwaka huu pia, Kanisa Katoliki duniani lilipata kiongozi mpya Papa Leo wa kumi nan ne, kufuatia kifo cha Papa Francis, huku kule Marekani mwanaharakati na mshirika wa Rais Trump Charlie Kirk akiuuwa kwa kupigwa risasi, tukio ambalo lilionekana kuigawa Marekani kwa misingi ya kisiasa.

Kabla ya mauaji ya Charlie Kirk, Rais Trump mwanzoni mwa mwaka huu alirejea katika Ikulu ya White House ambapo alianza kwa kutangaza vikwazo vya kiushuru kwa mataifa na kusitisha misaada ya nje matukio ambayo yametikisa dunia.

Licha ya wengi kuwa na matumaini katika mwaka mpya wa 2026, wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema huenda changamoto za kiuchumi ambazo zilionekana mwaka wa 2025 zikaendelea kuwepo hata mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *