Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF, linasema zaidi ya nusu ya watoto kwenye mji wa Um Baru huko Darfur Kaskazini, wanakabiliwa na utapiamlo, shirika hilo likisema hali inayoshuhudiwa ni mbaya kuwahi kurekodiwa duniani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa UNICEF utapiamlo miongoni wa watoto  umefikia asilimia  53 na kupita kiwango cha shirika la afya duniani  ambacho ni  asilimia 15 wakati huu mtoto mmoja kati ya sita waliochunguzwa nchini Sudan akipatikana kuwa na maradhi hayo, hali ambayo shirika hilo linataka uingiliaji kati wa haraka kuzuia vifo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Catherine Russell amesema hali hiyo imesababishwa na ongezeko kubwa la familia za wakimbizi wa ndani ambao walikimbia mapigano huko Al Fasher mwishoni mwa Oktoba, watoto chini ya miaka mitano wakichangia asilimia 26.

Aidha UNICEF imetoa wito kwa pande hasimu kwenye mzozo huo  kuruhusu ufikaji wa haraka  wa misaada ya kibinadamu na usalama wa wafanyakazi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *