Jeshi la Israel limetoa takwimu kuhusu kuangamizwa idadi kubwa zaidi ya wanajeshi wake mwaka huu wa 2025 unaoisha leo Jumatano na kutangaza kwamba 14% ya maangamizi hayo yametokana na vifo vya kujiua.

Televisheni ya Al Mayadeen imetangaza habari hiyo na kumnukuu Amir Bohbot, mchambuzi wa kijeshi wa tovuti ya Walla ya Israel akisema kuwa, mwaka 2025 ulikuwa mwaka wa umwagaji damu hasa na mkubwa kwa jeshi la Israel, na vifo vingi vimehusiana na vita huko Ghaza.

Ikumbukwe kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unachuja mno habari zake na kufikia kukiri kwamba mwaka 2025 ulikuwa mwaka wa maangamizi makubwa zaidi kwa wanajeshi wake, ni uthibitisho kuwa idadi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walioangamia ni kubwa kiasi kwamba Israel haiwezi tena kuficha. 

Jeshi la Israel limekiri kwamba idadi hiyo kubwa ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa inatia wasiwasi na kutangaza kuwa, juhudi zinaendelea za kupunguza matukio ya kujiua wanajeshi wa Israel na kuimarisha msaada wa kisaikolojia kwa wanajeshi.

Jeshi la Israel limetangaza kwamba, suala la kujiua wanajeshi wa Israel kutokana na misongo ya mawazo na kuchanganyikiwa ndilo linalozingatiwa zaidi hivi sasa.

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili mfululizo, jeshi la Israel liko vitani kuanzia huko Ghaza, mpaka katika nchi za Lebanon, Syria na Yemen.

Si hayo tu, lakini pia uchokozi wa Israel na Marekani katika vita vya siku 12 dhidi ya Iran uliilazimisha Tehran kutoa majibu na vipigo vikali kwa Israel na Marekani, masuala ambayo yamezidi kuwaweka kwenye hali mbaya ya kisaikolojia wanajeshi vamizi wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *