
Falme za Kiarabu zimetangaza siku ya Jumanne, Desemba 29, kuondoa wanajeshi wake kutoka Yemen, ikijibu makataa yaliyotolewa na Saudi Arabia. Mataifa hayo mawili ya kikanda yalikuwa washirika, kila moja ikiunga mkono vikosi vya Yemen vilivyopigana na waasi wa Houthi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wiki chache zilizopita, kundi la kusini linalotaka kujitenga, linaloungwa mkono na Falme za Kiarabu, liliteka sehemu kubwa ya eneo hilo kutoka kwa vikosi vinavyounga mkono Saudi Arabia na kusonga mbele hadi mpaka mrefu ambao Saudi Arabia inashiriki na Yemen. Vikosi hivi bado vinakataa kuondoka. Siku ya Jumanne Riyadh ilisema kwamba maendeleo haya yanatishia usalama wake wa kitaifa. Hivyo Abu Dhabi inaipinga Riyadh kwenye mipaka yake.
Baada ya siku nzima ya mvutano mkubwa, Falme za Kiarabu ziliamua kupitisha, angalau , mbinu ya upatanishi nchini Yemen. Saudi Arabia ilikuwa imewapa saa 24 kukubali kuondoa wanajeshi wao kutoka katika nchini hiyo, ambayo inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ushindani wa majirani zake ambazo ni nchi zenye nguvu katika ukanda huo. Jumanne, Desemba 30, Abu Dhabi ilitangaza kwamba jeshi lake lingeondoka Yemen.
Siku hiyo ilianza na shambulio la anga la Saudi Arabia dhidi ya meli iliyowasili Yemen kutoka Falme za Kiarabu. Katika hatua isiyo ya kawaida, mataifa hayo mawili yaliendelea na mawasiliano ya moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.
Riyadh inadai kulenga silaha na magari yaliyokusudiwa waasi wanaoungwa mkono na UAE. Abu Dhabi inasisitiza kwamba hakukuwa na silaha na kwamba magari hayo yalikusudiwa vikosi vya Imarati vinavyofanya kazi Yemen kwa uratibu na Riyadh.
Picha ya video kutoka kwa matangazo ya televisheni ya serikali ya Saudia siku ya Jumanne, Desemba 30, 2025, inaonyesha kile ambacho Riyadh zinakielezea kama shehena ya silaha na magari ya kivita kutoka Falme za Kiarabu, ikiwasili Mukalla, Yemen.
Kufuatia mvutano huu, Baraza la Rais wa Yemen linaloungwa mkono na Riyadh lilitangaza kufutwa kwa mkataba wa ulinzi na Abu Dhabi na kutangaza hali ya hatari ya kitaifa.
Ingawa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia kwa sasa hazielewani, zilikuwa washirika wa muda mrefu nchini Yemen dhidi ya waasi wa Houthi. Vikosi walivyoviunga mkono mtawalia vilikuwa vimeunda serikali ya mseto.
Lakini wiki chache zilizopita, kundi linalotaka kujitenga linaloungwa mkono na UAE, Baraza la Mpito la Kusini, lilichukuwa udhibiti wa eneo kubwa kutoka kwa vikosi vinavyoungwa mkono na Riyadh, na kusonga mbele hadi mpaka wa Saudi Arabia.
Ingawa Abu Dhabi imekubali ombi la kuondolewa kwa vikosi vyake, wapiganaji wanatotaka kujitenga wanakataa kusalimu amri. Kwa hivyo, mzozo huo unaweza kuendelea.
Sheria Mpya katika ushindani kati ya Abu Dhabi na Riyadh
Waangalizi wengi wameona kusonga mbele kwa kijeshi kwa Baraza la Mpito la Kusini kama kitendo kipya katika ushindani wa kikanda kati ya Abu Dhabi na Riyadh.
Yemen, kwa kweli, sio nchi pekee ambapo nchi hizi mbili zenye nguvu katika ukanda zinagombana. Kila moja ikiwa na mikakati tofauti.
Nchini Sudan, Falme za Kiarabu zinaunga mkono wanajeshi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Mwishoni mwa mwezi Oktoba, RSF iliteka jiji kuu la El Fasher katika shambulio la umwagaji damu dhidi ya jeshi la Sudan, ambalo linaungwa mkono na Riyadh.
Ilikuwa baada ya ziara ya Mwanamfalme wa Saudi Arabia katika Ikulu ya White House ambapo Washington iliwaomba “washirika” wa RSF kuacha kuwapa silaha.