Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara kupitia kitengo cha usalama barabarani limetoa wito kwa madereva wasio na sifa za kisheria kuendesha vyombo vya moto kuchukua hatua za kurejea darasani kwa mafunzo zaidi au kuachana kabisa na shughuli hiyo, huku msako mkali dhidi yao ukiendelea.
Wito huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoani humo wakati wa zoezi la ukaguzi wa madereva wa mabasi na malori yanayosafiri kati ya mikoa mbalimbali.
Amesema ukaguzi huo unalenga kudhibiti ajali za barabarani pamoja na kupunguza vitendo vya uvunjaji wa sheria za usalama barabarani vinavyofanywa na baadhi ya madereva, hususan wanaoendesha bila kuwa na sifa stahiki au kwa uzembe.
✍John Kasembe
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates